
Tetesi za soka Ulaya
Arsenal wamejiunga na Bayern Munich katika mbio za kumsajili kiungo wa Japan wa Brighton, Kaoru Mitoma mwenye umri wa miaka 28.
Mkurugenzi wa michezo wa Napoli, Giovanni Manna anatarajiwa kukutana na Manchester United kujadili uwezekano wa kumsajili winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20, Alejandro Garnacho, ambaye ofa yake ya pauni milioni 40 kutoka kwa mabingwa hao wa Italia ilikataliwa na Man Utd mwezi Januari.
Mshambuliaji wa Sweden, Viktor Gyokeres ataondoka Sporting msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa na Arsenal na Chelsea na ana makubaliano na klabu ya Ureno kumruhusu kuondoka chini ya kipengele chake cha kuvunja mkataba kwa pauni milioni 84.
Arsenal wanataka kipa wa Argentina wa Aston Villa, Emiliano Martinez, 32, arudi klabuni hapo huku Real Madrid wakimtaka kipa wa Arsenal Mhispania mwenye umri wa miaka 29, David Raya.
Msaidizi wa meneja wa Tottenham, Ryan Mason, ndiye anayeongoza katika orodha ya wanaowaniwa kuwa kocha mkuu wa West Brom.
Leicester City wametoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Guinea mwenye umri wa miaka 18, Abdoul Karim Traore kutoka klabu ya Ufaransa ya Bourg-en-Bresse.
Arsenal wanataka kiungo mkabaji wa Ghana, Thomas Partey abaki klabuni baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika msimu huu wa joto, licha ya kuhusishwa na kiungo wa Hispania wa Real Sociedad, Martin Zubimendi mwenye umri wa miaka 26.
Napoli wamempa kiungo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 33, Kevin de Bruyne, mshahara wa pauni milioni 23 kwa mkataba wa miaka mitatu kufuatia kuondoka kwake Manchester City msimu huu wa joto.